Na Timothy Itembe Mara.
MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara,Saimon Kiles ameongoza kikao cha baraza la bajeti kilicho pendekeza kubadili matumizi ya fedha shilingi milioni 301,270,626.19 zilizokuwa zimekasimiwa kununulia kuchimba visima vya maji na kuzielekeza katika manunuzi ya mtambo wa kulima barabara.
Akiongea mwenyekiti huyo alisema kuwa wananchi wa halmashauri ya Tarime na mkoa Mara kwa ujumla wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika mara kwa mara na wanatumia gharama kubwa pale ambapo wanawapa tenda mawakala katika matengenezo na kulima/kuzibua barabara.
“Madiwani wenzangu kamati ya fedha ilipendekeza bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha shilingi 301,270,627.19, kununua mitambo kwa ajili ya kuchimba visima vya maji,ununuzi wa gari na matengezo ya magari shilingi 150,712,165.4 kwa hali hiyo baraza nawaomba mridhie kiasi cha fedha hizo na nyingine zibadilishwe matumizi na zielekezwe katika matumizi ya najeti ya kununulia mitambo ya kulima miundombinu ya barabara ili kuondokana na kero iliyopo”alisema Kiles.
Mwenyekiti huyo aliongeza kusema mabadiliko hayo hayataadhiri mapendekezo ya kamati juu ya fedha tengwe za kulipa deni kiasi cha shilingi milioni 185 za MSD ili vituo vya kutolea huduma za Afya kupata dawa kadri watakavyokuwa wananunua/Agiza.
Pia mabadiliko hayo hayataadhiri mapendekezo ya kamati ya fedha iliyopendekeza ya rasimu ya mpango wa bajeti wa mapato na matumizi mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwemo fedha ya maendeleo ya vijiji na shuguli zingine za maendeleo kwa wananchi wetu.
Katika kokao hicho mwenyekiti huyo aliwaomba madiwani viti maalumu kufanya kazi ya kutembelea wananchi katika Tarafa watokanazo ili kuhamasisha maendeleo badala ya kujikita katika kata pekee wanazotoka.
Akiunga mkono hoja ya bajeti diwani viti maalumu,Ghati Chacha wa Tarafa ya Ichage alisema kuwa jambo hilo litasaidia kuwajenga wakina mama huku likiwatia joto la maendeleo pale ambao watakuwa wanatembelewa na madiwani wao na kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Diwani huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenzake pamoja na watumishi kushirikiana kwa pamoja katika swala zima la kuiletea maendeleo halmashauri ya Tarime .
Ghati aliwataka madiwani wenzake kwenda vijijini na kuwahamasisha wanawake kujiunga katika vikundi kwa lengo la kupata mikopo itokanayo na mapato ya makusanyo ya ndani asilimia 10 ambapo wanawake wanapata asilimai 4 na vijana asilimia 4 huku walemavu wakipata asilimia 2 mikopo isiyokuwa na riba.
Kwa upande wa halmashauri kaimu mkurugenzi wa siku hiyo,Peter Nyanja aliwa ahidi madiwani kuwa watumishi wake wataenda kuisimamia bajeti kama ilivyojadiliwa na kupitisha kwa maendeleo ya usitawai wa wanatarime.
0 Comments