F Mbunge wa Chalinze ampa heko Rais Magufuli kwa ujenzi wa Lambo Chamakweza Vigwaza | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbunge wa Chalinze ampa heko Rais Magufuli kwa ujenzi wa Lambo Chamakweza Vigwaza

 

NA ANDREW CHALE, CHALINZE.

MBUNGE Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa lambo kubwa kwa ajili ya mifugo ndani ya Kijiji 6cha Chamakweza Kata ya Vigwaza katika Halmashauri ya Chalinze, lililogharimu Tshs. Milioni 700.

Mbunge amebainisha hayo jana 24 Februari wakati wa ziara maalum ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul aliyetembelea kujionea lambo la mifugo linalojengwa chini ya Wizara yake hiyo sambamba na kuangalia miradi mingine ndani ya Halmashauri ya Chalinze. 

Akimpongeza kwa hatua hiyo, Ridhiwani Kikwete alisema:

"Niendelee kuishukuru Serikali kwa mambo makubwa na mazuri iliyotufanyia kwenye eneo letu hili la Chamakweza na Halmashauri yetu ya Chalinze kwa ujumla.

Mhe Naibu Waziri, katika bajeti ya miaka miwili iliyopita Serikali ilituidhinishia kiasi cha fedha Tshs Milioni 700 kwa ajili ya ujezi wa lambo hili." Alieleza Mbunge.

Mbunge aliongeza kuwa: 

"Serikali imeendelea kutoa fedha zingine ikiwemo Milioni 400 na nyingine Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuimalisha afya na ustawi wa mifugo yetu katika eneo ili la Chalinze.  

Yapo mambo mengi ambayo utayaona kwenye ziara yako leo. Lakini mimi nimesimama nikikushuru wewe kwa niaba ya Serikali yetu, lakini kwa upekee kabisa nimshukuru Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa namna moja ama nyingine ameendelea kuangalia mifugo kama sehemu kubwa ya  vitu au njia inayoweza msaidia Mtanzania kujiondoa kwenye wingu la umasikini.

Zipo njia nyingi sana lakini kikubwa imekuwa ikichangia pato la Serikali kwa zaidi ya asilimia 10 ambayo ni sehemu kubwa sana, kama mnavyofahamu sisi ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Afrika, tukiongozwa na wenzetu Waethiopia." Alisema Mbunge.

Aidha, Mbunge alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo pia anaamini zitafanyiwa kazi kwani Serikali iliyopo madarakani ni sikivu.

"Hapa ulipokuja Kijiji cha Chamakweza ni sehemu sahihi kwani asilimia kubwa ni wafugaji. Tunategemea utakuwa na msaada mkubwa sana kwetu sisi. Niendelee tena kumshukuru Mhe. Rais kwa jinsi ambavyo endelea kuingalia Chalinze na sisi Chalinze binafsi yetu tunamshukuru sana.

Mimi na Mwenyekiti wangu na Baraza letu la Madiwani tunapokutana kwenye vikao na kila siku hatuchoki kumuombea Mungu na aendelee kumpa nguvu, kumuongeza hekma na maarifa zaidi iliaendelee kuiangalia Chalinze kama sehemu ambayo inamuombea Mungu sana" Alimalizia Mbunge Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Kwa upande wake, Naibu Waziri  wa Mifugo na uvui Mhe. Pauline Gekul alibainisha kuwa, Wizara yake oliamua kutoa fedha hizo ili kutekeleza mradi huo ambao baada ya kukamilika utawanufaisha wananchi wa Chalinze hususani jamii ya wafugaji iliopo katika kijiji hicho cha Chamakweza. 

"Mradi huu ulitakiwa kukamilika tarehe 28.02. 2021 na mkandarasi anaetekeleza mradi akaomba muda wa wiki mbili hadi tarehe 10. 03. 2021 ili kumalizia sehemu ya asilimia iliobaki. Hivyo basi nawaomba sana wafugaji kuzuia mifugo yenu mbuzi, kondoo na ng'ombe kufika kwenye eneo la ujenzi kwa sasa. Tunawaomba mvumilie kwa siku 14 kutopeleka mifugo kule ili Mkandarasi afanye kazi zake kwa ubora amelize ndio patakuwa rasmi" alisema Naibu Waziri Gekul.

Aidha Naibu waziri alitoa salam za shukrani kutoka kwa Mh. Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wa Chalinze.

"Mhe. Rais anawashukuru sana wananchi wa Chalinze ndio maana Serikali imejipanga kuhakikisha wafugaji na wavuvi na wanannchi kwa ujumla wananufaika na mapato yatokanayo na kodi zinazotolewa na watanzania kitu kilichopelekea watenge bajeti kwa ajiri ya ujenzi wa bwawa hili la maji kwa matumizi ya kawaida na kunyweshea mifugo hapa Chamakweza". Alieleza Naibu waziri Gekul.

Aidha, alimtaka Mkandarasi kufanya kazi kwa ufanisi na kuzingatia muda aliopangiwa ili kukamilisha mradi huo kwa wakati huku pia kuona namna atakavyoongeza idadi ya birika za kunywea mifugo pasipo kuathiri ubora wa lambo hilo.

Post a Comment

0 Comments