F Mwalimu afa ndani ya tanki la maji | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwalimu afa ndani ya tanki la maji

 


Mwalimu wa Shule ya Msingi Michungwani wilayani Handeni, Athumani Nondo amekutwa amefariki akiwa ndani ya tenki la maji lililokuwa nje ya nyumba yake baada ya kutafutwa kwa siku mbili mfululizo.


Akielezea mkasa huo, diwani wa Kata ya Segera, Onesmo Makomero alisema taarifa walizopata ni kwamba Jumanne iliyopita marehemu aliondoka saa 2:30 usiku na familia yake haikujua alikoenda hivyo ikaanza kumtafuta bila mafanikio na Ijumaa mchana mwili wake ndani ya tanki.


“Mwili wa marehemu umekutwa Ijumaa majira ya saa saba mchana ndani ya Simtank lililopo nje ya nyumba yake,” alisema Onesmo.


Rafiki wa marehemu, Hassan Chambago alisema baada ya kumtafuta bila mafanikio “juzi, Ijumaa ilibidi tufanye dua maalum kumwombea maana ni muumini mwenzetu, baada ya dua tunatoka msikitini tukapewa taarifa kwamba marehemu amepatikana ndani ya tanki la maji,” alisema Chambago.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kuchunguza.

Post a Comment

0 Comments