F UWURA yatangaza kupanda kwa bei ya mafuta | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

UWURA yatangaza kupanda kwa bei ya mafuta


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya mafuta ya Petroli na Dizeli kutokana na kuongezeka kwa bei za mafuta katika Soko la Dunia na gharama za usafirishaji

Wanunuzi wa rejareja wa mafuta ya Petroli watatakiwa kuongezeka Tsh. 53 zaidi kwa lita, kuongeza Tsh. 134 zaidi lita ya Dizeli huku watumiaji wa Mafuta ya Taa wakitakiwa kuongeza Tsh. 119 kwa lita ikilinganishwa na bei ya mwezi Januari

Wanunuzi wa mafuta kwa jumla wataongeza Tsh. 52.90 kwa lita ya Petroli, Tsh. 133.36 kwa kila lita ya Dizeli na Tsh. 118.31 kwa kila lita ya Mafuta ya Taa


Post a Comment

0 Comments