F Bunge la jimbo la Virginia lafutilia mbali hukumu ya kifo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bunge la jimbo la Virginia lafutilia mbali hukumu ya kifo


Katika jimbo la Virginia nchini Marekani (USA), hukumu ya kifo ilifutiliwa mbali baada ya Wanademokrasia kushinda kwa wingi katika bunge la jimbo hilo.

Gavana wa Demokrasia Ralph Northern alitia saini muswada wa kupiga marufuku hukumu ya kifo, uliopitishwa na bunge la serikali na kusema "hili ni jambo la maadili kutekelezwa".

Virginia lililokuwa jimbo la 23 nchini humo kuchukuwa uamuzi huo, limekuwa jimbo la kwanza kupinga hukumu ya kifo kati ya majimbo ya kusini ambayo yamekuwa yakitekeleza adhabu hiyo mara kwa mara.

Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1608, jimbo la Virginia lilishika nafasi ya kwanza kati ya majimbo 50 nchini Marekani kwa kutekeleza takriban hukumu 1,400 za kifo.

Post a Comment

0 Comments