F Majonzi, Vilio Vyatawala Zanzibar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Majonzi, Vilio Vyatawala Zanzibar

 


Majonzi na vilio vimetawala visiwani Zanzibar wakati maelfu ya wananchi walipopata fursa ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli katika Uwanja wa Amaan leo hii ambapo shughuli ya kuuaga mwili huo ikiwa inaendelea.


Dk Magufuli alifariki dunia Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena iliyopo Jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo.


Mwili wa Dk Magufuli uliwasili visiwani humo saa 3:30 asubuhi katika  Uwanja wa Abeid Amani Karume na kupokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.


Maelfu ya watu walijitokeza pembezoni mwa barabara kutoka uwanjani hapo hadi Uwanja wa Amani uliopo Wilaya Mjini ambapo palifanyikana hafla nzima ya kumuaga mwili huo. 


Akitoa salamu za rambirambi, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema taifa limempoteza mwanamapinduzi mahiri na kumsifu Dk Magufuli kuwa alikuwa kiongozi mwenye uwezo na kipaji cha aina yake katika kuliongoza taifa.


Dk Mwinyi alieleza kuwa ni vigumu  kwa wakati huu kumpata kiongoz wa aina hiyo na kuwaomba watanzania kuendelea kumuombea dua na kumkumbuka kwa wema aliokuwa wake.


Akizungumza kabla ya kumkaribisha  Rais Dk Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa amesema kuwa mwili wake Dk Magufuli utalala Ikulu Zanzibar ambapo kesho asubuhi utasafirishwa kwa ndege maalum kuelekea Mwanza.


Aidha, Majaliwa amewapongeza Wazanzibar kwa namna walivyojitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa mpendwa wao hayati Dk Magufuli hata hivyo aliwashukuru waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahabarisha watu na kuongeza kuwa jana zaidi ya watu bilioni 3.9 duniani kote walifuatilia tukio la kumuaga Dk Magufuli.


Akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema wanzanzibar  wamedhihirisha umoja wao.


"Kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nishukuru sana wanzanzibar na serikali ya Zanzibar na kwamba uratibu huu wa kuuaga mwili huu wa Dk Magufuli umeshirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi,"alisema Mhagama.

Post a Comment

0 Comments