Netanyahu: Iran inahusika na mlipuko kwenye meli yake


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuhusika na mlipuko ndani ya meli inayomilikiwa na Israel katika Ghuba ya Oman. Hata hivyo, Netanyahu ameepuka kusema ikiwa Israel italipiza kisasi. 

Akizungumza leo na Radio Kan, waziri huyo mkuu wa Israel amesema ni wazi hiyo ilikuwa operesehani ya Iran. Meli hiyo ya mizigo iliyolipuka siku ya Ijumaa kwenye pwani ya Oman, jana ilikwenda katika bandari ya Dubai kwa ajili ya matengenezo.

 Haijafahamika wazi kilichosababisha mlipuko huo, lakini umetokea huku kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran wa mwaka 2015.

 Iran imekuwa ikiishinikiza serikali ya Rais Joe Biden kuipunguzia vikwazo ilivyowekewa chini ya mkataba huo na mataifa yenye nguvu duniani, ambao rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alijiondoa.

Post a Comment

0 Comments