Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Sharif amesisitiza mshikamano ili kutoathiri mabadiliko aliyoanza kuyaonyesha Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 5, 2021 wakati akizungumza na Wailamu waliojitokeza katika dua ya kumuombea marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.
Dua hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Mjini imefanyika katika msikiti wa Muembe Tanga Wilaya ya Mjini.
"Kwa sasa Wazanzibar tumempata Rais amejipambanua kuikwamua Zanzibar kutoka hapa ilipo, ipo haja ya kutazama mbele na kuyaacha makandokando nyuma," amesema
Amesema Maalim alikuwa muumini wa umoja na kwamba wakisimamia misingi hiyo watakuwa wamemtendea haki.
Naye makamu mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Juma Duni Haji amesema Maalim Seif alikuwa na lengo la kuwaunganisha na kuwatetea Wazanzibar.
0 Comments