F Rais Hussein Mwinyi afanya uteuzi wajumbe watatu wa baraza la wawailishi Zanzibar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais Hussein Mwinyi afanya uteuzi wajumbe watatu wa baraza la wawailishi Zanzibar


 Na Thabit Madai, Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wajumbe watatu wa baraza la wawailishi Zanzibar kuwa mawaziri katika wizara zilikuwa wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi, Mhandisi Zena A Said inasema kwamba kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya vifungu vya 42,43 (1)(2)na 44 vya katiba ya Zanzibar Rais wa Zanzibar Dk Mwinyi amemteuwa Dkt Saada Muya Saum kuwa waziri wa Nchi, Ofis ya makamu wa kwanza wa Rais.

Muya amekuwa mwakilishi wa kuteuliwa kwa nafasi ya rais na sasa anakuwa wazir atakae ongoza idara mbalimbali chini ya ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar.

Pia Dk Mwiyi amemteuwa Omar Said Shaabani kuwa wazir wa biashara na maendeleo ya viwanda pamoa na Nassor Ahmed Mazrui kuwa waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na watoto.

Zena amesema uteuzi huo umeanza leo rasmi machi 03, 2021 ambapo wateule hao wataapishwa hapo kesho tarehe 04 machi katika viwanja vya Ikulu Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Katika hafla hiyo ya kuwaapisha Mawaziri hao pia Rais atamuapisha Salum Yussuf Ali kuwa kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) ambae aliteuiwa tarehe 10 february 2021.

Uteuzi huo wa mawaziri unakamilisha safu ya baraza la mawaziri ambalo lilikuwa wazi kwa baadhi ya wizara kuwa wazi.


 

Post a Comment

0 Comments