F BAKWATA yatangaza tarehe ya Eid El-Fitr | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

BAKWATA yatangaza tarehe ya Eid El-Fitr

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewajulisha Waislamu na Wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr itakuwa Alhamisi Mae 13, 2021 au Ijumaa Mei 14, 2021.

Taarifa ya BAKWATA imefafanua sababu ya tarehe hizo mbili ni kutegemeana na kuandama kwa mwezi.

Sherehe za Eid El- fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam ambapo swala ya Eid itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi.

 

Post a Comment

0 Comments