F Dodoma Jiji kamili kuivaa Simba leo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dodoma Jiji kamili kuivaa Simba leo

 


TAYARI kikosi cha Dodoma Jiji ambao ni wapinzani wa Simba wapo ndani ya ardhi ya Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa leo, Uwanja wa Mkapa.

Jumla ya wachezaji 20, Benchi la ufundi pamoja na Viongozi wamewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo. 

Katika mchezo huo ni mtaalamu wa kucheka na nyavu Anuary Jabir pamoja na Rajab Mgalula ambao ni majeruhi wanatarajiwa kuukosa mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa huku wachezaji wote waliobakia wakiwa katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo.

Dodoma Jiji imetinga hatua ya Robo Fainali ikiwa na rekodi ya kuwa timu iliyofunga mabao mengi zaidi katika michuano hiyo msimu huu, ikifunga jumla ya mabao 14 katika michezo mitatu ambayo ilikuwa Dodoma Jiji 5 - 1 Hollywood FC, Dodoma Jiji 7 - 0 Kipigwe FC na Dodoma Jiji 2 - 0 KMC.

Post a Comment

0 Comments