F Lamine Moro aondolewa kikosini Yanga | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Lamine Moro aondolewa kikosini Yanga


Nadhoha wa Klabu ya Yanga, Lamine Moro ameondolewa kambini dakika za mwisho wakati kikosi cha wanajangwani hao kikijiwinda na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Namungo.

Nyota huyo raia wa Ghana, ameripotiwa kuondolewa kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu ambapo kocha wa Yanga, Mohamed Nabi ameamua kumuondoa ikiwa ni sehemu ya kumuwajibisha na iwe fundisho kwa wachezaji wengine.

Muda mchache baada ya kutajwa kuwa ameondolewa kikosini, Lamine Moro ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii,kuwa''Habari zenu, tafadhali kama umesikia chochote kuhusu mtu fulani hebu jaribu kuuliza  ni kipi kinaendelea kabla haujasema chochote kuhusu mtu huyo'' ameandika Lamine kupitia Instagram .

Yanga ambayo ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama 57, inasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Namungo katika Ligi Kuu kwakuwa mara zote tatu walizokutana mechi zao zilimalizika kwa sare.


 


 

Post a Comment

0 Comments