Chuo kikuu cha Dar es salaam kimetakiwa kupanua wigo wa Wiki ya Utafiti ili kushirikisha watafiti ambao tafiti zao zimesajiliwa na zina uhusiano na idara mbalimbali za kitaaluma chuo hapo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako wakati akifunga kilele cha Maadhimisho ya 6 ya Wiki ya Utafiti na ubunifu sambamba na utoaji wa Tuzo kwa washindi katika ubunifu,utafiti na huduma za jamii ambayo yamefanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Dkt Akwilapo amesema Wizara ya elimu itaendelea kuunga mkono maadhimisho hayo kwani yanaleta matokeo chanya katika utafiti kwa kuwa kivutio kwa wadau wautafiti lakini pia kusaidia kuimarisha ushirikiano na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi.
Awali akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof.William Anangisiye amesema katika kutoa msukumo kwenye utafiti na ubunfu Chuo hicho kimetenga fedha kwa ajili ya utafiti pamoja na ubunifu.
Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI ambaye pia ni mratibu wa maadhimisho hayo Prof.Benadeta Killian ameeleza vitendo mbalimbali ambavyo vimejipatia tuzo ni pamoja na mtafiti bora na mradi bora wa huduma za jamii na mbunifu bora mwaka 2021.
Maadhimisho hayo ya utafiti ya siku tatu yalianza Mei,24 mpaka 26 ambapo yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na alitumia fursa hiyo kuvitaka vyuo vikuu vyote nchini kuweka utaratibu wa kufanya utafiti na kisha kuonesha matokeo ya tafiti ili kusaidia kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya vyuo na soko la ajira.
0 Comments