Na Hamisi Nasri, Masasi.
WAFANYABIASHARA zaidi ya 600 wa soko kuu la mkuti wilayani Masasi mkoani Mtwara wametangaza mgomo kutolipa ushuru wa mabanda wanayofanyia biashara zao kwa halmashauri ya mji Masasi kutokana na kutokuwa na imani na wakusanyaji wa ushuru wa halmashauri.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa wakusanyaji wa ushuru wa halmashauri hiyo wamekuwa wakiwabambikizia madeni hewa pamoja na kuwatoza ushuru kiholela na kutopatiwa risiti pale wanapolipa ushuru wa mabanda yao.
Mgomo huo waliutangaza rasmi jana mjini Masasi wakiwa kwenye mkutano wao dhalura wa umoja wa wafanyabiashara wa soko hilo la mkuti, mkutano ambao ulilenga kukutana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Masasi,Gimbana Ntavyo ambaye hata hivyo mkurugenzi huyo akujitokeza katika mkutano huo.
Wakizungumza katika mkutano huo wafanyabiashara hao walisema kuwa kuanzia jana Mei tano na kuendelea wanatangaza rasmi mgomo wa kutolipa ushuru wa aina yoyote ukiwemo ule wa mabanda.
Gistusi Joseph mfanyabiashara soko kuu la mkuti alisema kwa sababu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi ameshindwa kufika katika mkutano huo kwa ajili ya kuwasilikiza wafanyabiashara hao juu ya kero zao wanaungana pamoja katika mgomo huo.
"Tumekuwa tukiandikia madeni hewa na kulipishwa ushuru bila ya kupewa risiti na wakusanyaji wa ushuru wa halmashauri yetu sasa kwa jambo hili tunatangaza kutolipa ushuru," alisema Joseph
Zaurati Khamisi mfanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa ameshangazwa kuona ameandikiwa madai ya deni katika banda lake kuwa anadaiwa kiasi cha sh zaidi ya.300,000 wakati deni lake halisi analodaiwa ni sh.30,000 ambalo ni deni la miezi mitatu na kwamba ushuru wa fedha za miezi iliyopita aliyolipa hajapewa risiti ya malipo aliyoyalipa licha ya kuomba risiti hizo kwa muda mrefu kutoka kwa wakusanyaji hao wa ushuru wa halmashauri.
Alisema kutokana na kero hizo na kitendo cha mkurugenzi wa halmashauri mara kadhaa kushindwa kufika katika vikao vya wafanyabiashara hao kusikiliza na kumaliza mgogoro huo wao kama wafanyabiashara sasa wameona ni bora wasitishe kulipa ushuru wa mabanda hadi pale mkuruenzi huyo atakapokutana na wafanyabiashara ili kumaliza malalamiko yao.
Naye alisema
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa soko hilo na umoja wa wafanyabiashara was soko, Abdalah Mtandama alisema wameomba kukutana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili kufikisha malalamiko yao na yapatiwe ufumbuzi.
Alisema wafanyabiashara wa soko hilo wameandikia barua na ofisi ya mkurugenzi kudaiwa madeni ya ushuru wa mabanda madeni ambayo sio sahihi.
"Tulimuita mkurugenzi aje hapa na wakusanyaji wake wa ushuru ili tumuambie kama madeni ambayo wametuandikia sio sahihi na wakusanyaji watuambie fedha zetu tulizokuwa tukilipa wamepeleka wapi," alisema Mtandama
Mtandama wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao hawana deni na halmashauri lakini wameandikiwa madeni jambo ambalo sio sahihi.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi, Gimbana Ntavyo alisema alipokea barua kutoka kwa wafanyabiashara wao ya kumtaka kuudhulia mkutano huo.
Alisema kama wafanyabiashara hao wanamadai juu kutozwa ushuru bila ya kupewa risiti na kubambikiziwa madeni ni bora wakaenda ofisini kujieleza juu ya malalamiko yao.
0 Comments