F Wanajeshi wa Marekani wameondoka Kandahar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wanajeshi wa Marekani wameondoka Kandahar

 


Maafisa wa kijeshi wa Marekani wamesema kuwa nchi hiyo imekamilisha kazi ya kuwaondoa wanajeshi wake wote kutoka kambi ya anga ya Kandahar kusini mwa Afghanistan, ambayo iliwahi kuwa ya pili kwa ukubwa miongoni mwa vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Afghanistan.


Wiki iliyopita, jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi kutokea kambi hiyo, kulisaidia jeshi la serikali ya Afghanistan kuhimili kishindo cha shambuliokubwa la Wataliban. Msemaji wa jeshi la Afghanistan mkoani Kandahar, Khoja Yaya Alawi amelithibitishia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi wote wa Marekani wamekwishaihama kambi. 


Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kandahar amesema jeshi la Marekani litaikabidhi kambi hiyo Jumamosi baada ya kumalizika kwa sherehe za Eid -Ul- Fitr. Afisa mmoja wa jeshi la Afghanistan ambaye hakupenda jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la AFP kuwa kuondoka huko kwa Marekani kunawaacha katika hali dhaifu.

Post a Comment

0 Comments