BALOZI Mdogo wa China aliopo Zanzibar Zhang Zhisheng amesema ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China utaendelea kuimarika kutokana na udugu wa muda mrefu uliopo .
Kauli hiyo ameitoa wakati akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Dkt. Omar Dadi Shajak huko ofisini kwake mnazimmoja
Amesema vifaa hivyo vitasaidia katika utoaji wa huduma mbali mbali ikiwemo barakoa pamoja na mitungi ya hewa ya oxygen kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja pamoja na Hospitali ya Abdalla Mzee ilioko pemba.
Aidha alisema mashirikiano ya pamoja yanahitajika ili kupambana na wimbi la tatu la Covid-19, ambalo linaonyesha kuathiri duniani kote .
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Dkt. Omar Dadi Shajak alimshukuru Balozi huyo kwa kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuipatia vifaa hivyo pamoja na misaada mengine wanayoisaidia ikiwemo kuwapatia Madaktari Wataalamu wa Maradhi mbali mbali .
Aliahidi kuitumia vizuri misaada hiyo ambayo itasaidia katika kupambana na maradhi ya covid 19 kwa wananchi wa Zanzibar .
Aliwasisistiza wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi ya korona kwa kuvaa barakoa ,kunawa mikono mara kwa mara pamoja kuepukana na mikusanyiko isio ya lazima .
Wakati huo huo Dkt Shajak alipokea msaada wa mashine ya kupumulia kutoka kwa shirika la Japiego kupitia kwa Mkurugenzi wa afya Laurel Fain kutoka Marekeni.
0 Comments