Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri.
Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha kiungo hicho.
Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C.
Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binaadamu, kwani hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni.
Pia, kitunguu maji ni chanzo cha madini mengi ambayo yanapatikana katika kiungo hicho ambayo yana umuhimu mkubwa katika mwili wa binaadamu.
Licha ya kuwa na umuhimu huo, pia huimarisha afya ya moyo, kuzuia kansa, huukinga mwili dhidi ya vidonda vya tumbo, huongeza joto mwilini na huzuia vimelea vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binaadamu.
Faida za kitunguu maji katika mwili wa binaadamu ni pamoja na kuupa mwili nishati, kuongeza nguvu, huimarisha misuli ya mwili, huongeza hamu ya kula, hulainisha tumbo na kuondoa tatizo la kukosa choo.
Pia faida nyingine ya kitunguu ni kuwa kinatibu pumu, uvimbe wa pafu, saratani, majipu, mvilio wa damu, kufungua choo, kupunguza uzito na chunusi.
Kitunguu maji kinaweza kutengenezewa juisi kwa kukikatakata ma kisha kukisaga kwa blenda kwa kuchanganya na maji ya kunywa mara unapojisikia vibaya hasa kwa watu ambao wanasumbuliwa na kifua mara kwa mara.
Pia unaweza kuchanganya na asali na kunywa nayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kutibu maumivu ya tumbo na uvimbe mwilini. Maji ya kitunguu kwa mujibu wa wataalamu wa tiba wanasema yanatibu matatizo ya macho.
0 Comments