F Kikosi cha Timu ya KMC FC kuwafuata Dodoma Jiji kesho | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kikosi cha Timu ya KMC FC kuwafuata Dodoma Jiji kesho


Kikosi cha Timu ya KMC FC, kitaondoka Jijini Dar es Salaam kesho kuelekea Jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Juni 17 katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.

Kikosi hicho cha wana Kino Boys kinachonolewa na kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo, kimekuwa na maandalizi kwa muda mrefu kuelekea katika mchezo huo ambapo pamoja na mambo mengine ilijikita kuhakikisha kwamba inafanya vizuri katika michezo iliyosalia.

KMC FC inakwenda kukutana na Dodoma Jiji ugenini katika mchezo wa pili ambapo awali kwenye duru ya kwanza ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi  wa magoli mawili kwa sifuri na kwamba kuelekea katika mchezo huo, imejipanga kuondoka na alama tatu licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni,inatambua ubora wa Timu ya Dodoma jiji inapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini KMC FC ikobora zaidi kwenye kuhakikisha mkakati wakuchukua pointi tatu unafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Leo tumefanya maandalizi ya mwisho kabla ya safari yetu ya kwenda Dodoma kesho kwenye mchezo muhimu dhidi ya Dodoma Jiji, tumefanya maandalizi yakutosha kabisa, hivyo tunakwenda kuendeleza kile ambacho awali tulikifanya, lakini pia tunafahamu Dodoma Jiji inauwezo mzuri, lakini KMC FC pia nibora zaidi, kikubwa tunakwenda kupamba kupata alama tatu ilituendelee kusalia kwenye nafasi nzuri ambayo hivi sasa tunaihitaji.

KMC FC inahitaji kufanya vizuri katika mchezo huo ili kubaki kwenye nafasi ya kuwania nafasi ya Nne ambapo hivi sasa ipo kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 41, huku ikicheza michezo 29 nakusaliwa na michezo mitano kabla ya kumalizika kwa Msimu wa 2020/2021.

Michezo hiyo ni Dhidi ya Dodoma Jiji ambapo KMC FC itakuwa ugenini,  Mtibwa Sugar, JKT Tanzania, Simba pamoja na Ihefu ambapo yote watakuwa wenyeji.

Post a Comment

0 Comments