Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, ametangaza kuwa yuko tayari kuipatia Korea Kaskazini chanjo ya corona (Covid-19).
Kulingana na ripoti ya NK News, Moon alifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Austria Van der Bellen ambapo alisema,
"Ikiwa Korea Kaskazini itakubali, nitashirikiana kikamilifu kuwapa chanjo ya Covid-19."
Moon pia alisema kuwa kuondoa hatari zote za janga la Covid-19 inawezekana iwapo kutakuwa na uzingatiaji wa haki wa kutoa chanjo kote ulimwenguni.
Rais wa Austria Van der Bellen naye alieleza kuwa hana uhakika juu ya msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu misaada ya chanjo, lakini ikiwa utawala utakubali, basi bila shaka misaada itatolewa.
Pendekezo la Moon la misaada ya chanjo bado haijapata jibu kutoka Korea Kaskazini.
0 Comments