F RC Mtaka amekitaka chama cha wafugaji mkoa wa Dodoma kupeleka mpango kazi wao | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

RC Mtaka amekitaka chama cha wafugaji mkoa wa Dodoma kupeleka mpango kazi wao


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameuagiza uongozi wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Dodoma kumpelekea mpango kazi wa chama hicho kwani Mkoa huo una mifugo mingapi huku akiwataka wafugaji wa Mkoa huo kufuga kwa tija ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza jijini Dodoma na viongozi wa chama cha wafugaji kanda ya kati wakati akijitambulisha kwa  wafugaji wa huo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka amesema

uongozi wa Mkoa lazima upeleke mpango kazi wao siku ya Ijumaa ofsini kwake ili kuona mwelekeo na mpangio wa chama hicho.

"Kumbukeni nyinyi ni wafugaji wa makao Makuu ya nchi nitashangaa sana endapo nitaona wafugaji kutoka Mikoa mingine wanakuja kuchangamkia fursa la soko katika Mkoa wetu wa Dodoma

"Nitawakutanisha na wataalamu kutoka Wizara ya mifugo ili wawafundishe mbinu bora za ufungaji mifugo wa mifugo michache ila wenye faidi nyingi ," amesema Mtaka.

Mtaka ameongeza kuwa “Mkoa una mifugo mingapi Wilaya ipi ina mifugo mingi, nani ana mifugo mingi ili awasaidie kukutana na wataalamu waweze kufuga kwa tija kuliko ufugaji wa sasa” amesema Mtaka.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa  amewataka wafugaji kuwapeleka watoto wao shule na kuacha utaratibu wa kuwafanya watoto wao kuwa ndio wachungaji wa mifugo kwani jambo hilo ni baya na hataki litokee katika mkoa wake.

“Wenzenu wana mifugo lakini wanaochunga mifugo wanatoka mbali na watoto wao wanakwenda shule, utakuta mtoto wa mfugaji mwenzio mwalimu, Profesa, lakini wako ni mchungaji hilo sitaki kusikia” amesema.

Amesema kuwa na  mifugo mingi ni utajiri hivyo wafugaji wanatakiwa kufuga kwa tija ili iweze kuwanufaisha ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule watoto wao.

Ameongeza kuwa "Itakuwa haina maana kuona mfugaji anamsululu wa mifugo lakini bado ni masikini wa kutupwa naomba mtambue kwamba Mfugaji wa leo ni yule mwenye maendeleo mwenye nyumba ya kisasa na watoto wake wote wenye umri wa kwenda  shule wanakwenda shule " amesema Mtaka.

Awali Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Mkoa wa Dodoma Reginaldo Lubeleje  akisoma  risala kwa niaba ya wafugaji  katika mkutano huo amemuomba Mkuu huyo kuwatatulia migogoro ukwemo ule wa  pori la akiba la Mkungunero na wananchi wa Wilaya za Kondoa na Chemba.

Pia, amesema wanakabiliwa na changamoto za migogoro ya mipaka, kutokuwa na soko la uhakika,kutokuwa na elimu ya ufugaji, uhaba wa maji pamoja na watendaji kuuza maeneo yao ya malisho.

Naye, Mfugaji kutoka Wilayani Kondoa Sadick Hassan, amesema  changamoto yao kubwa wanayokabiliana nayo wafugaji  ni pamoja na Majosho na kutokuwepo kwa sehemu ya malisho ya mifugo yao hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu.


 

Post a Comment

0 Comments