F Serikali yawapandisha madaraja Watumishi 70,437 ,Yatenga Bilioni 300 kwa ajili ya mishahara mipya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali yawapandisha madaraja Watumishi 70,437 ,Yatenga Bilioni 300 kwa ajili ya mishahara mipya

SERIKALI imewapandisha madaraja watumishi wa umma 70,437 nchini huku ikitenga shilingi bilioni 300 kwa ajili ya mishahara mipya itakayoanza kulipwa kuanzia mwezi June 2021.

Hayo yamebainishwa leo June 21,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohammed Mchengerwa wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Idara wa Utawala na Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma.


Mhe.Mchengerwa amesema kuwa  taratibu zote za upandishaji zinaendelea na watumishi hao waliopanda vyeo watapata mshahara wa mwezi  huu kulingana na madaraja yao waliyopandishwa

’Watumishi 70,437 waliopandishwa  madaraja, jumla ya Sh. Billioni 300 Rais wetu mama Samia Suluhu Hassani ametoa kwa ajili ya kuwapatia mishahara mipya inayoanza kulipwa mwisho wa mwezi huu, alisema Waziri huyo’’, amesema Mchengerwa

Waziri amesema kuwa watumishi 11,983 wenye malimbikizo serikalini watalipwa malimbikizo ya mishahara yao kwani wamekuwa wakiendelea na uchunguzi na kupitia madai yao.

”Serikali imetenga Sh. 23,781 bilioni kuhakikisha wanawalipa malimbikizo watumishi hao ambapo ofisi yake imeshafanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba ni kweli wanadai malimbikizo yao”

Waziri Mchengelewa amesema kuwa Rais ameshatoa fedha hizo hivyo malimbikizo ya watumishi hao nao watalipwa mwisho wa mwezi huu.

Hata hivyo amesema kuwa  Rais Samia ameshatoa kibali cha kupandisha madaraja watumishi 91841 hivyo watumishi wote wenye sifa ya kupandishwa madaraja watapandishwa na kupewa haki yao.

Pamoja na serikali kutimiza wajibu wake kwa watumishi hao ikiwamo kuwapandisha madaraja na kulipa malimbikizo yao serikali inawakumbusha watumishi kuendelea kuwatumikia wananchi kwa Uadilifu na vinginevyo watachukuliwa hatua.


Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa wakuu wa idara wanakazi kubwa ya kuhakikisha watumishi wanaowasimamia wanatimiza majukumu yao na wajibu wao hivyo kama maafisa utumishi wakawe kioo kwa wanao waongoza na jamii zao kwa ujumla.

 

Post a Comment

0 Comments