Mahakama ya Israel imeamua kumwachilia huru Sheikh Kamal al-Hatib, ambaye ni Makamu wa Rais wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ya 1948.
Kulingana na taarifa ya shirika rasmi la utangazaji la Israel KAN, jaji wa Mahakama Kuu ya wilaya ya Nazareth alikataa ombi lililowasilishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuchelewesha kutolewa kwa Hatib kwa masaa mengine 48.
Hatib, ambaye aliachiliwa chini ya masharti maalum, alipigwa marufuku "kuhojiana, kutoa mahubiri au kuzungumza na jamii, kwenda katika mji wa Kefr Kanna, ambao ni makazi yake kwa siku 45, kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, na kuhudhuria mikusanyiko ya zaidi ya watu 15."
Mwanasheria Mkuu wa Israel alimshtumu Hatib kwa "uanachama katika shirika lililopigwa marufuku na kuchochea vurugu", akiashiria Harakati ya Kiislamu ya 1948.
Sheikh Hatib, ambaye pia ni raia wa Israel na anaongoza Tume ya Uhuru ndani ya Kamati Kuu ya Ufuatiliaji ya Waarabu (YATK), ambayo inawakilisha Wapalestina, alizuiliwa nyumbani kwake katika mji wa Kefr Kanna kaskazini mwa Israel mnamo tarehe 14 Mei.
Kipindi cha kizuizini cha Hatib, ambaye alifikishwa mahakamani siku moja baada ya kuwekwa kukamatwa, kiliongezewa tarehe tofauti kwa sababu mbalimbali.
0 Comments