Kanisa la Mhubiri Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza siku na mahali atakapozikwa.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN, lilisema Mhubiri TB Joshua atazikwa karibu na makao yake makuu mjini Lagos.
Mhubiri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
"Tunajiandaa kwa ibada ya kila wiki kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua." taarifa ilisema.
TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.
TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.
Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.
TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Amerika Kusini.
0 Comments