MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi leo Juni 8 ametinga makau makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuchukua fomu ya kugombea urais wa TFF.
Mkwabi amekwenda kuchukua fomu hiyo kwa niaba ya mgombea Wallace Karia ambaye yeye ndiye mgombea wa nafasi hiyo.
Karia yupo madarakani kwa sasa katika ngazi ya Urais hivyo anahitaji kutetea nafasi yake kwa wakati mwingine tena.
Zoezi la utoaji fomu limeanza leo ambapo zinatolewa makao makuu ya TFF, Karume na fomu zinapatikana kupitia tovuti ya TFF.
Mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha ni saa 10:00 Juni 12 mwaka huu.
0 Comments