Wazalishaji Wa Mbegu Za Pamba Kunufaika Na Ongezeko La Bei Kuanzia Mwakani

 


NA TIGANYA VINCENT RS TABORA

SERIKALI imesema kuanzia msimu ujaoa wakulima wa pamba katika maeneo ya uzalishaji wa mbegu watanufaika na ongezeko   asilimia kuanzia 10 hadi 20 ya bei iliyotangazwa(bei dira).


Kauli hiyo imetolewa jana Wilayani Igunga na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya masoko ya pamba na kuhamasisha wakulima wa zao hilo kulima kwa wingi alizeti, choroko, dengu na pamba yenye.


"Kuanzia msimu ujao Wilaya ya Igunga na Tanganyika ambazo zinahusika na uzalishaji wa mbegu za pamba kwa ajili ya wakulima wa maeneo mengine nchini watapata 'additional incentive' kwa kuongezewa bei" alisema

 

Alisema mnunuzi yote wa pamba atakayekwenda kununua zao hilo atakakiwa kutoa bei ya ziada ili kuwafanya wakulima wa maeneo hayo ambao ndio wanatunza mbegu waweze kupata pesa tofauti na maeneo mengine yanalima zao hilo.


Aidha Bashe aliwahakikisha wakulima wa pamba wa Igunga kuwa Kitalu cha uzalishaji wa mbegu za pamba hakitahamishwa  kitabaki wilayani humo.



Katika hatua nyingine Bashe ameagiza Bodi ya Pamba nchini kuangalia uwezekano wa kutafua njia ya kukikopesha Chama cha Msingi cha Ushirika cha Igunga Balimi AMCOS Matreka matatu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa pamba.


Alisema matreka hayo yanaweza kuwekewa utaratibu mzuri ambapo wanachama watakuwa wakikodisha kwa ajili ya kuwawezesha kulima mashamba makubwa.


Wakati huo huo Bashe alisema kuanzia msimu ujao wa kilimo  Serikali itagawa mavazi rasmi ya kuvunia pamba na kuhifadhi pamba ili kuhakikisha inakuwa na ubora wa hali ya juu.


Alisema mifuko ya kuhifadhia itakuwa ya aina mbili ya kuweka pamba ya kiwango cha juu na mwingine wa kuweka ya kiwango cha chini.


Bashe alisema sanjari na hilo mifuko hiyo itakuwa na namba za utambulisho wa mkulima ili kama kutatokea dosari waweze kutambua mhusika na kumchukulia hatua yeye.

Post a Comment

0 Comments