Na Victor Masangu, Bagamoyo.
WAZIRI wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amechukizwa na kukemea vikali vitendo vya baadhi ya maafisa elimu wa Mikoa na Wilaya kuwa na tabia ya kufanya udanganyifu sababu ambayo inapelekea hali ya sintofahamu kwa wadau elimu wa Tanzania na kuwataka kubadilika na kusimamia ipasavyo sera pamoja na mitaala iliyopo kwa lengo la kuweza kukuza sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo.
Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi rami wa mafunzo maalumu ya siku nne ya uthibiti ubora wa ndani kwa kwa maafisa elimu wote wa Mikoa 26,maafisa elimu wa taaluma wa Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi kutoka halmashauri mbali mbali yaliyofanyika katika ukumbi wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM) Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Pia aliwaagiza maafisa elimu hao kuweka mipango madhubuti katika sualazima la kusimamia fedha za umma zinazotolewa na serikali katia kutekeleza miradi mbali mbali iliyopo katika sekta ya elimu na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inaweka mazingira mazuri ya wanafunzi na kuboresha elimu katika ngazi zote.
“Kuna maagizo ambayo tayari yametolew na Rais wetu wa awamu ya sita wakati analihutubia bunge kwa hivyo hili ni agizo kwa kwamba yale yote ambayo yamesema inatakiwa tufafanyie kazi ipasavyo na sio mpaka msubilie mimi niwape taarifa na hili ni kwa lengo la kuweza kuleta mabadikilo chanya katia sekta yetu ya elimu na kwamba haya mafunzo myatumia vema uko mnapokwenda na mimi ninawashukuru sana uongozi wa Adem katika kusimamia vema suala la elimu,alisema Ndalichako.
Awali Afisa mtendaji mkuu wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM) Dr. Siston Mgullah akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo hayo ambapo amesema yamewashirikisha maafisa elimu Mkoa, maafisa elimu taalamu Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi katika halmashauri mbali mbali kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa ujuzi katika suala zima la kusimamia uthibiti ubora wa elimu.
Dr. Mgullah aliongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa kipindi cha muda wa siku nne lengo lake kubwa ni kuwajengea umahiri zaidi katika kuboresha elimu sambamba na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika kuchapa kazi kwa bidii lengo ikiwa ni kutimiza malengo ya kukuza sekta ya elimu hapa nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washiriki wote wa mafunzo haya pamoja na kuwashukuru wakufunzi mbali mbali wa Wakala wa ADEM kwa maandaliziambayo wameyafanya katika kutimiza jambo hili pamoja na Waziri wa elimu kuja kwa ajili ya kutufungulia rasmi mafunzo haya katika mafunzo haya,”alisema. Mgullah.
Halhaji Abdul Maulid ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam amebainisha kwamba kufanyika kwa mafunzo hayo ya uthibiti ubora kutaweza kuwa mkombozi mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika kuongeza zaidi kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi sambamba na uwajibikaji na ujuzi katika kuboresha sekta ya elimu.
Pia Afisa elimu huyo alifafanua kwamba baada ya kumalizika mafunzo hayo yataweza kuwapa fursa ya kubadilishana uzoefu na maafisa elimu wengine kutoka mikoa mbali mbali na kwamba atahakikisha anaweka mipango imara na madhiubuti katika kusimamia ipasavyo maelekezo yote amabyo yametolewa na waziri wa elimu kwa kuyafanyia kazi kwa vitendo.
“Kwanza sisi kama wasimamizi wa elimu na mimi kama Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaishukuru serikali pamoja na Adem kwa kuweza kutukutanisha kwa pamoja maafisa elimu wa mikoa yote ya Tanzania, maafisa elimu wanaosimamia elimu ya msingi pamoja na wataalamu wengine hii maana yake sasa tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kuleta mageuzi katika sualala uhibiti ubora wa elimu na nina imani tutafanikiwa,’alifafanua Maulid.
Kwa upande wake Afisa elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Shomari Bane ambaye anasimamia elimu ya msingi amesema kuwa mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo mkubwa katika suala zima la kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwamba yataweza kuwaongezea ujuzi na umahiri katika kutoa huduma ya elimu inavyotakiwa kwa wanafunzi.
Pia Afisa huyo alisema kwamba baada ya mafunzo hayo yataweza kwenda kuleta mabadiliko chanya katika suala zima la uthibiti ubora wa elimu, pamoja na kusimamia ipasavyo jinsi ya mwenendo mzima wa mitaala ya elimu inayotumika kwa sasa lengo na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ambayo yametolewa na Waziri wa elimu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewahasa walimu hao wakuu kutumia fursa waliyoipata kwa kuhakikisha wanatembelea vivutia mbali mbali vya utalii na makumbusho yaliyopo kwa lengo la kujifunza mambo mabli mbali ya kihistoria ambayo yataweza kuwasaidia pindi wanapofundisha somo la historia.
0 Comments