F Waziri Ummy: Tumeshawapandisha madaraja walimu 1135 kwa halmashauri ya Mwanza | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Waziri Ummy: Tumeshawapandisha madaraja walimu 1135 kwa halmashauri ya Mwanza

 


Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu, amesema tayari wameshawapandisha madaraja walimu 1135 kwa halmashauri ya Mwanza kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1/05/2021 alipokuwa Mwanza

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wannachi wa Butimba katika ziara ya Rais wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza.

Mhe. Ummy amesema hayo katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, inayoendelea Jijini Mwanza leo, Juni 14, 2021 ambapo amesema Rais Mhe. Samia ni mtu anayetekeleza yale yote anayoyaahidi kwa wananchi wake.

"Mhe Rais alikuwa hapa tarehe 1/5/2021 akatuelekeza tupandishe madaraja walimu wote wa msingi na sekondari tumetekeleza ahadi yako walimu wote waliostahili kupanda madaraja katika halmashauri ya Mwanza 1135 wamepandishwa madaraja maana yake kuna utulivu katika shule zetu, watoto watasoma bila shida," amesema Waziri Ummy.

Pia, Mhe. Ummy amesema katika kuhakikisha elimu inazidi kukua tayari kuanzia mwezi Machi 2021 Rais ameshatoa shilingi bilioni 3.9 kwa ajaili ya kuboresha elimu katika mkoa wa Mwanza huku TAMISEMI ikiwa imeleta shilingi milioni 500 kwa ajili ya hospitali ya Nyamagana.

Post a Comment

0 Comments