Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imethibitisha kumshikilia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa mahojiano.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amesema kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia.
"Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda Ng'anzi
0 Comments