F Madaraja 15 Makubwa au Marefu zaidi Duniani | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Madaraja 15 Makubwa au Marefu zaidi Duniani

 

Kwa siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa maendeleo makubwa katika shughuli mbalimbali za binadamu. Sekta ya ujenzi na usafiri ni moja kati ya sekta ambazo binadamu amepiga hatua kubwa.

Kila siku kumekuwa kukibuniwa na kufanyika maboresho mbalimbali katika miundombinu ya usafirishaji. Kumeshuhudiwa ujenzi wa barabara za kisasa, reli, viwanja vya ndege au hata kubuniwa kwa baadhi ya aina mpya za usafiri.

Kutokana na hili, yapo madaraja mbalimbali yaliyojengwa sehemu mbalimbali duniani ili kuboresha usafiri wa barabara na reli. Karibu uongeze maarifa yako kwa kufahamu madaraja 15 makubwa au marefu zaidi duniani kwa sasa.

1. Daraja la Danyang–Kunshan


Daraja la Danyang–Kunshan ndilo daraja refu kuliko yote duniani, lina urefu wa kilometa 164.8. Daraja hili linapatikana huko China kati ya  Beijing–Shanghai na lilikamilika kujengwa mwaka 2010. Daraja hili hutumiwa na treni ya umeme inayokwenda kasi.

2. Daraja la Changhua-Kaohsiung

Changhua-Kaohsiung ni daraja la pili kwa urefu duniani linalopatikana huko Taiwan. Daraja hili lina urefu wa kilometa 157.3, lilikamilika mwaka 2007 na linatumiwa na treni ya umeme ya kasi kubwa.

3. Daraja la Tianjin


Daraja la Tianjin linaunganisha Langfang na Qingxian katika njia ya treni ya mwendokasi ya Beijing–Shanghai huko China. Daraja hili ni moja kati ya madaraja marefu duniani kwani lina urefu wa kilometa 113.7.


4. Daraja la Cangde

(Picha haikupatikana)


Daraja hili limejengwa kwenye njia ya treni ya kasi kubwa ya Beijing – Shanghai huko China. Daraja hili lina urefu wa kilometa 105.8 na limejengwa kwa mfumo ambao linaweza kustahimili matetemeko; lilikamilika mnamo mwaka 2010.

5. Daraja la Weinan Weihe


Hili ni daraja linalopatikana katika njia ya treni ya kasi kubwa ya  Zhengzhou–Xi’an huko China. Daraja hili lina urefu wa kilometa 79.6 na linakatiza mto Wei mara mbili, mito mingine kadhaa, barabara kadhaa pamoja na njia kadhaa za treni.

6. Daraja la Bang Na Expressway

Hili ni daraja linalobeba barabara kubwa ya juu na lina urefu wa kilometa 55. Daraja hili linapatikana huko nchini Thailand na linakatiza mto Bang Pakong.

7. Daraja Kuu la Beijing

Daraja hili lina urefu wa kilometa 48.15 na linapatikana huko China. Daraja hili linatumiwa na treni za kasi kubwa zinazofanya safari kati ya Beijing – Shanghai.

8. Daraja la  ziwa Pontchartrain Causeway

Hili ndilo daraja linaloaminika kuwa refu zaidi huko Marekani na moja kati ya madaraja marefu yanayokatiza juu ya maji duniani.

Daraja hili linahusisha madaraja mawili yanayokatiza ziwa  Pontchartrain kusini mwa Louisiana yakiwa na urefu wa kilometa 38.35.

9. Daraja la Manchac Swamp

Hili ni daraja linalohusisha madaraja mawili pacha yaliyojengwa kwa zege huko Lousiana Marekani. Daraja hili linakatiza ziwa Pontchartrain na lina urefu wa kilometa 36.69.

10. Daraja la Hangzhou

Daraja la Hangzhou ni daraja la treni linalopatikana huko china na lina urefu wa kilometa 35.67.

11. Daraja la Runyang

Runyang ni daraja kubwa linalokatiza mto  Yangtze katika jimbo la Jiangsu huko China. Daraja hili lina urefu wa kilometa 35.66 na linaunganisha sehemu ya kusini ya Zhenjiang na ya kaskazini ya Yangzhou mwa mto Yangtze. Daraja hili ni sehemu ya njia ya mwendokasi ya Beijing-Shanghai.

12. Daraja la Donghai

Daraja la Donghai ni moja kati ya madaraja marefu zaidi duniani yanayokatiza bahari. Daraja hili lina urefu wa kilometa 32.5 na linaunganisha Shanghai na bandari ya kina kirefu ya Yangshan huko China.

13. Daraja la Shanghai Maglev

Hili ni daraja la treni ya juu linalotoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pudong hadi kwenye viunga vya pembezoni vya mji wa Shanghai huko China.

Njia hii huwafikisha wasafiri mahali ambapo wanaweza kupata usafiri wa chini ya ardhi wa kuelekea watakako. Daraja hili lina urefu wa kilometa 29.9

14. Daraja la Atchafalaya

Atchafalaya ni daraja linalopatikana huko nchini Marekani na lina urefu wa kilometa 29.29. Atchafalaya ni daraja la tatu kwa urefu huko nchini Marekani na la 14 duniani.

15. Daraja la ghuba ya Jiaozhou


Hili ni daraja linalopatikana katika jimbo la Shandong huko China likiwa na urefu wa kilometa 26.7. Mnamo mwezi Disemba mwaka 2012 daraja la Jiaozhou liwekwa kwenye rekodi za dunia za madaraja marefu zaidi yaliyoko juu ya maji.

Hitimisho

Kwa hakika kuna madaraja mengi zaidi ya haya, lakini nimekuorodheshea haya 15 marefu na makubwa zaidi duniani. Naamini umejifunza mengi pamoja na kufurahia makala hii.


Post a Comment

0 Comments