Rais Xi Jinping asifu mafanikio ya China na kuonya kuhusu nguvu kutoka nje

 


Rais wa China Xi Jinping leo ameyaonya mataifa ya kigeni dhidi ya kujaribu kuionea China akisema enzi za kufanya hivyo zimepitwa na kwamba taifa hilo la kikomunisti limechukua mwelekeo wa kujiimarisha na "kutorudi nyuma". 

Xi ameyatoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 100 tangu kuundwa kwa chama cha kikomunisti cha China ambacho kimeliongoza taifa hilo la mashariki ya mbali kwa zaidi ya miaka 70. 

Kwenye sherehe hizo zilizoandaliwa kwa mtindo wa kuonesha nguvu za China, Xi ameahidi kuimarisha nguvu za kijeshi za taifa hilo, kukirejesha kisiwa cha Taiwan chini ya himaya ya China pamoja na kuimarisha nafasi ya Beijing katika uendeshaji wa mji wa Hong Kong.


Post a Comment

0 Comments