F Serikali yapeleka Sh500milioni kujenga kituo cha afya Maisome | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali yapeleka Sh500milioni kujenga kituo cha afya Maisome


Ili kuwaondolea adha akina mama wajawazito kupoteza maisha kwa kukosa huduma ya afya hasa kwenye kisiwa cha Maisome, Serikali imepeleka Sh500milioni kwa ajili ya kujenga kituo cha afya kwenye kisiwa hicho.


Mbunge wa jimbo la Buchosa, Erick Shigongo ameyasema hayo Julai 18 mwaka huu kwenye mkutano wa  hadhara uliofanyika Kijiji cha Kanoni  Kata ya Maisome.


Amesema kumekuwepo na vifo vya akina mama hasa  wakati wa kujifungua nanaposafiri umbali mrefu kuvuka maji umbali wa kilometa 68 kutokana Maisome hadi Sengerema mjini kupata huduma hiyo wengi wao hupoteza maisha.


Hivyo Serikali imeona ni vema kuwasadia wananchi wa kisiwa cha Maisome kupata kituo cha afya ili kuondokana na adha hiyo.


"Tunaishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo wananchi wa Maisome watakuwa wamepata suluhisho la tatizo linalotolakana na vifo vya akina mama na mtoto " amesema Shigongo.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda amesema kupitia vikao mbalimbali vya wananchi pamoja na wataalamu wataamua kituo hicho cha afya kijengwe kijiji gani ambapo itakuwa rahisi kupata huduma.


Anastazia John Mkazi wa Kijiji cha Kanoni amesema Serikali imefanya jambo jema ambalo litasaidia wananchi wa kisiwa cha Maisome kuondokana na kuvuka maji kutafuta huduma ya afya

Post a Comment

0 Comments