F Shirika la haki za binadamu lazindua ripoti ya haki za binadamu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Shirika la haki za binadamu lazindua ripoti ya haki za binadamu

Shirika la haki za binadamu "Legal and Human Right Centre 'LHRC' limezindua ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu inayohusu Haki za Binadamu na Biashara 2021.

Shirika hilo limegundua kuwa Wafanyakazi wengi hawapewi fedha za ziada kwenye masaa ya ziada na wengine kutokulipwa kabisa wanapokuwa wamefanyakazi kupita kiasi, kwani kuna makampuni watu wanafanya kazi masaa 12 au masaa 13 mpaka 14 lakini sheria inasema mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi masaa 8 kwa siku na masaa 40 kwa wiki.


Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC bibi Anna Henga amesema wamegundua kuwa wafanyakazi aslimia 59  hawana mikataba ya ajira, Na amehaidi kuipeleka ripoti hiyo kwenye Taasisi za udhibiti wa Fidia, Wizara ya Ajira, Wizara ya uwekezaji na Wizara ya Ardhi

Kwa upande mwingine ameiomba serikali hasa kupitia Taasisi za udhibiti watembelee makampuni na viwanda mbalimbali na kuangalia jinsi gani wanaheshimu haki za binadamu.

 

Post a Comment

0 Comments