F Taasisi sita za Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari zajifungia Dodoma kujadili ripoti ya CAG | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Taasisi sita za Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari zajifungia Dodoma kujadili ripoti ya CAG

TAASISI sita za Wizara ya Mawasilino na Teknolojia ya Habari zimekutana Jijini Dodoma lengo likiwa ni kujadili  jinsi ya uandaaji wa vitabu vya Hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akifungua kikao kazi hicho,leo Julai 29,2021,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasilino na Teknolojia ya Habari,Dkt.Zainabu Chaula amesema wameamua kwa pamoja wakae kupeana AB kwani mwaka jana walikuwa hawajafanya vizuri na  kulikuwa na sintofahamu katika Taasisi mbili.

 


“Hichi kikao tulikipanga na ni cha mkakati kwa sababu masuala ya ukaguzi yapo kisheria katika Taasisi sita zinapaswa pia kufuata sheria hizo kazi ya kiongozi ni kuhakikisha kanuni,taratibu na sheria zinafuatwa binadamu bila kumfuata kwa karibu tegemea kufeli,”amesema.

“Katika Taasisi wapo waliofanya vizuri lakini wapo waliokuwa na Kwere za kutosha na kweli mara nyingi tunazitengeneza wenyewe kwahiyo wao kama wahasibu wa ndani ambao tumewapa jicho la kwanza haya ni maandalizi ili mkaguzi mkuu wa Serikali akija akute mambo yamekaa sawa sio kwa kutengeneza tunataka kutengeneza utamaduni huu,”amesema.

Amesema wameamua kuweka utaratibu huo kwa sababu mara nyingi wanapokuja wakaguzi wanakuta baadhi ya vitu havipo sawa hivyo wanatengeneza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja.

“Tunatengeza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja,kwa sababu mara nyingi wanapokuja wakaguzi wanakuta baadhi ya vitu havipo natamani kuna mambo mengine ni ya msingi lakini hatuyatekelezi sasa hapa nimekuja kuwaambia nini tunatarajia na wamekuja wahasibu na wakaguzi wa ndani wao ndio wanapaswa kuwasaidia,”amesema Katibu Mkuu.


Kwa upande wake Mkaguzi  wa ndani Mkuu wa Wizara ya Mawasilino,Teknolojia ya Habari,CPA Joyce Christopher amesema wapo kwa ajili ya kikao kazi ambapo Taasisi sita zimejumuika wakiwemo  wakaguzi wa ndani na wahasibu ambapo lengo ni kupanga mipango ya pamoja jinsi ya kufunga mwaka.

Amesema agenda ya pili ni  utekelezaji wa hoja zilizoibuliwa na  CAG na  kuzifanyia kazi ili ziweze kufungwa mwaka 2020-2021 asikute hoja.

“Majukumu ya kitengo cha ndani katika kuhakikisha hoja za CAG zinafanyiwa kazi  lengo ni kuboresha na kuhakikisha tunafanya vizuri pia kuangalia thamani ya fedha za Serikali zinaonekana,”amesema CPA Joyce.


Naye,Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka  Shirika la Mawasilino Tanzania  (TTCL) Octavian Barnabas amesema lengo la kikao hicho ni kupunguza hoja zilizotokana na Ofisi ya  CAG ambapo kwa  pamoja wataibuka na majibu nini kifanyike ili kusiwe na kwere.

 

Post a Comment

0 Comments