F Yanga kumuaga rasmi Niyonzima leo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Yanga kumuaga rasmi Niyonzima leo

 


KIUNGO Haruna Niyonzima ataagwa rasmi na klabu yake ya Yanga leo Julai 15 watakapomenyana na Ihefu FC ya Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo alitua nchini na kuanza kuitumikia Yanga kwenye msimu wa mwaka 2011/2012 na kufanikiwa kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu akiwa na Yanga na mawili akiwa na Simba SC.

Yanga imepanga kuutumia mchezo wa leo kumuaga mkongwe huyo ambaye ana uwezo wa kuuchezea mpira kwenye miguu yake namna ambavyo anataka na ukamtii.

Kwa sasa Ihefu ina alama 35 kwenye msimamo wa ligi ikiwa nafasi ya 15, huku waliopo chini yake ni Gwambina FC na Coastal Union wenye pointi 34 kila timu.

Ihefu inazihitaji alama tatu kutoka kwa Yanga ili kuzivuta shati Mbeya City na JKT Tanzania wenye pointi 36 kila moja.

Yanga inahitaji kushinda mtanange huo ili kumuaga vema kiungo huyo aliyerejea klabuni hapo Januari, 2020 nyakati za dirisha dogo na mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Simba Januari 4, 2020, iliyomalizika kwa sare ya 2-2.

Msimu huu nyota huyo ni mechi 13 amecheza ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo timu yake imekusanya jumla ya pointi 70.


 

Post a Comment

0 Comments