F Ahukumiwa kifungo na faini baada ya kukutwa na silaha nzito aina ya kifaru nyumbani kwake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ahukumiwa kifungo na faini baada ya kukutwa na silaha nzito aina ya kifaru nyumbani kwake

 Mstaafu mmoja nchini Ujerumani ametiwa hatiani kwa kosa la kumiliki silaha baada ya kubainika kuwa na silaha kubwa binafsi kikiwemo kifaru.

Mtuhumiwa huyo ,84, amehukumiwa kifungo cha miezi 14 na ameamriwa kulipa faini ya pauni 213,469.

Maafisa walibaini kifaru na vifaa vingine vya kijeshi vya enzi ya vita vya pili vya dunia kwenye makazi ya mzee huyo katika mji wa Heikendorf mwaka 2015

Jeshi lilisaidia kuondoa vifaa hivyo.

Jumatatu, mahakama iliamuru kuwa mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikutajwa kwasababu ya sheria ya faragha ya Ujerumani, lazima auze au akigawe kifaru hicho na silaha ya kupambana na mashambulizi ya anga iwekwe kwenye makumbusho

Kwa mujibu wa wakili wa mtuhumiwa, idara ya makumbusho ya Marekaniina nia ya kununua kifaru.

Wanahistoria wengi wa Marekani wanasema kilikuwa kifaa bora zaidi kilichotumiwa na Ujerumani wakati wa vita vya pili vya dunia.

Mwanasheria amesema kuwa maafisa wanaokusanya vifaa vya kijeshi wa Ujerumani walitaka silaha nyingine kama vile bunduki na bastola, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.

Mamlaka za mji huo zilivamia makazi yake mwaka 2015 baada yakupata taarifa kuhusu vitu vinavyomilikiwa na mstaafu huyo, taarifa hiyo ilitolewa na wafanyakazi wenzao wa Berlin, ambao awali walifanya upekuzinyumbani kwake wakitafuta mchoro ulioibiwa baada ya enzi za Nazi.

Wanajeshi kama 20 hivi walitumia saa tisa kukiondoa kifaru hicho kutoka kwenye makazi ya mstaafu huyo

Vyombo vya habari vya huko viliripoti kwamba mtu huyo alikuwa ameonekana wakati mmoja wa baridi akitumia kifaru kama jembe la kuondolea barafu.

Post a Comment

0 Comments