F Chama cha Harakati ya Ennahda nchini Tunisia chamtaka Rais Kays Said kurudi kwenye mchakato wa katiba | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Chama cha Harakati ya Ennahda nchini Tunisia chamtaka Rais Kays Said kurudi kwenye mchakato wa katiba

Chama cha Harakati ya Ennahda nchini Tunisia kilimtaka Rais Kays Said, ambaye alifanya maamuzi kama vile kumfuta kazi waziri mkuu na kusimamisha mamlaka ya bunge, "kurudi kwenye mchakato wa katiba".

Katika taarifa iliyoandikwa kutoka kwa Harakati ya Ennahda, ilielezwa kuwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Bodi ya Utendaji ya chama hicho, Rais Said wa Tunisia alitathmini migogoro mingi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na afya ambazo nchi ilikuwa ikipitia, akizingatia "hatua za ajabu za mapinduzi".

Kwa kusisitiza kuwa kipaumbele cha taasisi za serikali na muundo wa kisiasa nchini Tunisia ni kuangalia shida za kiafya na kiuchumi za Watunisia, taarifa hiyo pia ilisema,

"Mbinu zinazotumiwa na Rais ni kinyume cha katiba na inakiuka sheria. Ni shambulizi la demokrasia, haki za raia na za kibinafsi za watu wa Tunisia, zikiburuza taasisi za serikali kwenye mzozo ambao unawazuia kufanya kazi zao kutumikia nchi na serikali pamoja na raia."

Harakati ya Ennahda inasema kuwa maamuzi ya Rais, ambayo "yanaonyeshwa kama mahitaji halali na watu kama njia ya kutoka kwa msukosuko, hayawezi kutoa suluhisho kwa shida zilizokusanywa na ugumu wa hali, na badala yake, zinaweza kuathiri utulivu , usalama wa kijamii na kiuchumi wa watu, na hivyo kuongeza mateso ya Watunisia."

Katika taarifa hiyo, Harakati ya Ennahda ilimtaka Rais wa Tunisia "kuweka masilahi ya nchi mbele, kurudi kwenye mchakato wa katiba, kutenda kazi kulingana na sheria, na kufungua nafasi ya mazungumzo ya kitaifa ambapo kila mtu atakubali matokeo."

Taarifa hiyo pia iliomba raia wote kushikamana na demokrasia na kusimama dhidi ya machafuko, vurugu na hujuma.

 

Post a Comment

0 Comments