MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani amewataka Wakazi wa Mkoa huo kutumia ujenzi wa bomba la mafuta na Reli ya kisasa kama fursa ya kujipatia maendeleo kupitia huduma mbalimbali watakazozitoa kwa mafundi.
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga.
Balozi Dkt.Batilda amesema kuwa wakazi wa Tabora wanatakiwa kutumia miradi hiyo katika kuzalisha mazao ya aina mbalimbali na kuboresha ufugaji kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mafundi wakati wa ujenzi.
Amewataka viongozi katika Wilaya zote za Mkoa wa Tabora kuanza kuwaandaa wananchi kwa kutoa elimu juu ya manufaa ya miradi hiyo na umuhimu wa wao kushiriki kama sehemu ya kujipatia fedha kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema wameanza mikakati ya kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya chini kwa kuunda Polisi jamii nagzi za Kata ili kuweka mazingira mazuri na salama kwa wawekezaji katika miradi hiyo.
Amewataka wakazi wa Tanzania kushirikiana na Vyombo vya ulinzi katika kuimarisha usalama katika maeneo yote ya Mkoa wa Tabora ili kuwavutia wawekezaji,
0 Comments