Rais mpya wa Iran, Ebrahim Raisi, leo hii amesema serikali yake itachukua hatua kadhaa kwa lengo la kuviondoa vile alivyoviita vikwazo vya kidhalimu vilivyowekwa na Marekani.
Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa madhehebu ya Shia, ameyasema hayo muda mfupi baada ya kupata ridhaa ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, katika hafla iliyofanyika mjini Tehran.
Amesema ataboresha hali ya uchumi, ambao kwa kiasi kikubwa umevurugwa na vikwazo vya Marekani vya tangu 2018, ikiwa ni baada ya Marekani kuyatelekeza makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015, yaliyoyajumuisha mataifa mengine makubwa sita duniani.
0 Comments