Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima amelitaka Shirikisho la Soka nchini 'TFF'na viongozi wa mikoa katika mpira kukutana na kuzungumza kwa pamoja juu ya misingi ya kuendesha mchezo huo kisasa kuliko kubahatisha.
RC Malima ameyasema hayo leo Agosti 7, 2021 wakati anazungumza akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa TFF kabla ya uchaguzi huo kufanyika lengo likiwa ni kuchochea mabadiliko ya uendeshwaji wa soka na kuwa kisasa zaidi.
“Shirikisho la soka nchini 'TFF'na viongozi wa mikoa katika mpira wakazungumze kwa pamoja kuona ni namna gani misingi ya mpira wa kisasa unaendeshwa kuliko kubahatisha kama tunavyoona hivi sasa tuna wachezaji huko Urutuki na Morocco, inabidi tuwekeze kwenye soka la vijana”. Alisema Adam Malima Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Vilie vile amesifia mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa mpira wa miguu ndani ya miaka 25 iliyopitana tunapaswa kuendelea na kasi ili kupiga hatua Dunia nzima.
Kiongozi huyo ni mdau mkubwa soka nchini kwani alionesha mchango mkubwa wa kuisaidia klabu ya Biashara United Mara kwa kupelekea umoja kwa viongozi, wadau na mashabiki wa klabu hiyo pamoja na misaada ya kifedha ambayo yote kwa pamoja imechangia klabu hiyo kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu na kukata tiketi ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho Africa ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya timu hiyo.
0 Comments