Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy
Mwalimu amelazimika kuigeuza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani
Shinyanga kuwa sehemu ya Shamba darasa kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa kote nchini.
Hatua
hiyo ya Waziri Ummy imewafikisha viongozi hao katika miradi ya
uwezeshaji ya wananchi kiuchumi kwenye eneo la Chapulwa, lenye ukubwa wa
hekari 2000 huku hekari 90 zikiwa zimetolewa kwa mwekezaji, na katika
eneo la Zongomera lenye hekari 2100, Hekari huku 500 zimegawanywa bure
kwa wajasiriamali ili waendeshe shughuli za kibiashara na ufundi.
Wakionekana
kuguswa na hatua zilizochukuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama,
yakuwawezesha wanachi kujikwamua kiuchumi, wakuu hao wa Mikoa wameaahidi
kutumia fursa ya maarifa waliyopokea kwaajili ya Mikoa yao.
Akiongea
kwa niaba ya wakuu wa Mikoa wenzake, Mwenyekiti wa wakuu wa Mikoa Mhe.
John Mongella, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amesema ziara hiyo
imewafungua macho, hivyo watachukua hatua za haraka katika kufanikisha
azma hiyo kwakuwawezesha wananchi kwenye maeneo yao.
“Mhe.
Waziri, Mimi kwa niaba ya viongozi wenzangu hatuna lakusema kwa sasa,
ila tumuahidi Mhe. Rais kwamba, tunakwenda kuishi viapo vyetu, moja
ikiwa nikuhakikisha maarifa haya ambayo wenzetu wa Kahama tumevuna kwao,
sisi tutakwenda kufanya vizuri zaidi” alisema Mongella.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adamu Malima, hakusita kuonesha
hisia zake mbele ya Waziri Ummy na kutoa maelekezo ya haraka kwa Katibu
Tawala wa Mkoa huo, kuhakikisha manunuzi ya Jozi tatu za Masofa ambazo
zilikuwa zimepangwa kununuliwa na Ofisi hiyo ya Mkuu wa Mkoa kwenye
maeneo mengine, sasa manunuzi hayo yafanyike kwenye kampuni ya *Wahitime
Furniture* ya Kahama Shinyanga ilioanzisha kiwanda cha Furniture katika
eneo hilo la biashara ikiwa ni jitihada zakuunga Mkono shughuli hiyo
inayofanywa na vijana wazalendo wa kitanzania.
Awali
akitoa maelezo Mbele ya Waziri wa Nchi na Ujumbe wake, Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba, alisema wao kama Manispaa walikaa
na kuamua kutoa Hekari 500 bure kwa wananchi, lakini mara baada ya Mradi
kuanza, sasa Halmashauri inakusanya shilingi Milioni. 80 kila mwaka,
fedha inayoingia kama sehemu ya mapato ya ndani.
0 Comments