Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umeandaa maonyesho ya biashara yanayofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 8 Oktoba, 2021 katika Kituo cha Biashara cha Wernhil (Wernhil Shopping Mall) kilichopo mjini Windhoek. Maonesho haya muhimu katika utelezaji wa Diplomasia ya Uchumi yanalenga kutangaza bidhaa za Tanzania na Utalii nchini humo ili kukuza biashara na kuvutia wawekezaji nchini.
Katika maonesho hayo Ubalozi umewashirikisha Watanzania wajisiriamali na wafanyabiashara waishio nchini humo (diaspora) ambao wamejitokeza kuonesha bidhaa mbalimbali ikiwemo mchele, korosho, kahawa, asali, majani ya chai, maharagwe, vitenge, batiki na nguo za kufuma.
Sambamba na kunesha bidhaa maonyesho haya yamejumuisha uuzaji wa vyakula mbalimbali vya kitanzania ambavyo vimekuwa vivutio kwa wateja wengi.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba tarehe 4 Oktoba 2020.
0 Comments