F ECOWAS yapitisha vikwazo vikali dhidi ya utawala wa kijeshi Mali | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

ECOWAS yapitisha vikwazo vikali dhidi ya utawala wa kijeshi Mali


Jumuiya ya Kiuchumi Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, imekutana katika mkutano wa usio wa kawaida mjini Accra, Ghana, siku ya Jumapili na kuidhinisha maamuzi yaliyochukuliwa na Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) saa chache kabla.


Nchi za Afrika Magharibi zimeamua kuzuia mali ya nchi ya Mali inayowekwa katika benki ya BCEAO, kufunga mipaka kati ya Mali na nchi wanachama wa ECOWAS lakini pia kusimamisha shughuli za kiuchumi na Bamako isipokuwa bidhaa za matibabu na muhimu. ECOWAS pia imeamua kuwaondoa mabalozi kutoka nchi zote wanachama nchini Mali pamoja na vikwazo vingine kuhusu usaidizi wa kifedha.

Post a Comment

0 Comments