Hamad Masoud Hamad ametangaza rasmi kujiondoa ACT

 


Na THABIT MADAI, ZANZIBAR.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT - WAZALENDO Eng Hamad Masoud Hamad ametangaza rasmi kujiondoa ndani ya Chama hicho  kuanzia Leo February 08,2020 kwa kile anachodai kufanyiwa udhalilishaji katika kipindi cha Uchaguzi wa ndani wa Chama hicho.


Hamad Masoud ametoa Uwamuzi huo leo Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi Airport Saccos uliopo kiembe Samaki Mjini Unguja.


Alisema kuna mambo mengi yalimtokea katika Uchaguzi huo ambayo yalimdhalilisha ikiwemo kuambiwa kumuua mkewe kwa sababu ya kushinda nafasi ya Mwenyekiti.


Alisema katika Uchaguzi huo haukuwa Huru na Haki kwani alikuwa hashinani na Juma Duni Bali alikuwa akishindana na uongozi mzima wa Chama cha ACT WAZALENDO.


"Katika jinai nilioifanya mimi kigombea nafasi ya Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO Taifa, Chama kilikuwa kimegawanyika na Viongozi wa Juu Walikuwa na Mgombea wao,hivyo Mimi sikuwa nashindana na Babu Duni nilikuwa nashindana na Chama," Alieleza.


Alifafanua kuwa " Kama kungekuwa na Uchaguzi wa Huru na Haki ndani  ya ACT WAZALENDO basi Babu  Duni asingepata hata Asilimia 20,"


Hata hivyo alisema kwa sasa Bado hajaamua atahamia Chama kipi ila kwa sasa tayari ameshalewa maombi ya Vyama Nane kuhamia katika Vyama vyao.


Hamadi katika Uchaguzi huo Hamad Masoud alipata kura 125 sawa na Asilimia 26.94 huku Juma Duni Haji alipata kura 339 sawa na Asilimia 73.06.


Post a Comment

0 Comments