Mkulima mmoja nchini Benin, Baraka Amidou (37), amepokea tuzo ya heshima kutoka kwa mamlaka ya nchi yake, baada ya kukabidhi begi lenye mamilioni ya pesa kwa mmiliki wake, aliloliokota wakati akitokea shamba kuelekea nyumbani.
Amidou amesema kwamba uamuzi huo wa kurejesha fedha hizo, ulichochewa na imani na malezi ya kidini na kusema wala hajutii alichokifanya na begi hilo lilikuwa ni la mfanyabiashara aliyefika katika eneo hilo kununua mazao.
Akizungumza wakati akimkabidhi tuzo na zawadi zake, Gavana wa Borgou Kaskazini mwa Benin Djibril Mama Cissé, alisema, "Siku hizi tunazidi kushuhudia upotevu wa maadili, haijapata kutokea kijana ambaye bado ana kila kitu cha kufanya ili kujijenga akafanya kitendo kama hicho”.
0 Comments