Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali zitakazohusika kwenye droo hiyo itakayochezeshwa kesho ni Mabingwa watetezi Chelsea, mabingwa mara 6 Liverpool, Manchester City zote za England, mabingwa wa kihistoria Real Madrid, Atletico Madrid, Villarreal zote za Hispania, timu nyingine na Bayern Munich ya Ujerumani ambao ni mabingwa mara 6 wa michuano hii na Benfica kutoka nchini Ureno.
Katika droo hiyo itapangwa michezo ya hatua ya robo fainali pamoja na nusu fainali lakini pia itapangwa ratiba ya timu zipi zitaanzia nyumbani na zile zitakazoanzia ugenini. Hii ni droo ya wazi ambapo timu kutoka taifa moja zinaweza kukutana kwenye hatua hii hivyo timu yoyote kati ya hizo 8 inaweza kukutana na timu yoyote.
Mchezaji wa Zamani wa vilabu vya Inter Milan, Manchester united, Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Mikael Silvester ambaye ni mshindi wa michuano hii ya Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2008 akiwa na Manchester United ndiye atakayechezesha droo hiyo.
Michezo ya robo fainali ya mkondo wa kwanza itachezwa kati ya Aprili 5 na 6 na ile ya mkondo wa pili itachezwa Aprilii 12 na 13. Michezo ya nusu fainali mkondo wa kwanza itachezwa Aprili 26 na 27 na ya mkondo wa pili itachezwa Mei 3 na 4. Na mchezo wa fainali kwa msimu huu wa 2021-22 inafanyika nchini Ufaransa katika Dimba la Stade de France Jijini Paris Mei 28 2022.
0 Comments