F Kilimo bora cha viazi vitamu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kilimo bora cha viazi vitamu

 



Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma.

Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji.

Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista.

Faida:
vina wanga, vitamin, kambalishe, madini ya kalisiuamu, potasiamu, chuma, protini, na kalori.

Uzalishaji 
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.

Namna ya kuandaa ardhi:
Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.

Ukuaji wa viazi huathirika kama kiwango cha oksijeni kwenye udongo si cha kutosheleza, mifereji na ulimaji wa matuta makubwa ni muhimu, safisha ardhi mapema kwa kuondoa magugu, lima mara kwa mara ili kulainisha udongo.

Upandaji:
kupanda ni kwa kutumia mbegu halisi za viazi, usipande sehemu zenye maji mengi maaana mbegu zinaweza kuoza,hifadhi kwenye sehemu yenye baridi kidogo na giza mpaka mbegu zitakapoota, kadri upandavyo viazi vikubwa, ndivyo mavuno yatakuwa mengi, Tengeneza matuta ya kupandia yaliyoinuka.

Kitalu kilichopandiswa juu hutoa mavuno Zaidi, panda mbegu nzima au kata katika vipande viwili kabla ya kupandda,ziache mbegu kwa wiki moja ili zitoe vifundo, panda vipande vya mbegu umbali wa inchi 10-12 kati ya mbegu moja na nyingine na fukia katika shimo la urefu wa inchi 1 hadi 3, mfumo  wa upandaji kwa mstari mmoja au miwili unaweza tumika,  iwapo mfumo wa mstari mmoja utatumika acha nafasi ya inchi 24 mpaka 36 kati ya mstari hadi mstari na ikiwa mfumo wa mistari miwili utatumika acha nafasi ya inchi 70 kabla ya mstari mwingine.

Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu.

Palizi:
palilia mara tu magugu yatakapoonekana na wakati huohuo ondoa baadhi ya miche iliyoota karibu karibu ili kutengeneza nafasi, funika nyufa ardhini kwa udongo ili kuzuia wdudu. Baada ya mimea ya viazi kuota, unaweza kutandaza majani ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kushamiri na kupoza udongo.

Wadudu na magonjwa.
Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV),ukurutu ugonjwa usabababishao unyaukaji na kifo cha tishu za kiazi ( potato blight), kuoza shingo (Bacteria soft Rot), minyoo fundo ( Root notes Nematodes), uozo wa kahawia ( Brown Rot).

Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango.

Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta.

Post a Comment

0 Comments