Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urais wa Tanzania leo Alhamisi Machi 24, 2022 amefunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Doreen amesema baada ya ndoa hiyo takatifu, ahadi yake ni kuzidi kumpendezesha Mrema kutoka hapo alipo hadi kuwa kijana.
“Kwanza watu waelewe kwamba mpaka kufikia wanamuona hivi, mimi ndio nimefanya hivi, kwani katika kipindi hiki cha uchumba nilikuwa nikimlea kwa muda mrefu sasa kuhakikisha anakuwa sawa na vitu vyote anavyovihitaji anavipata na anapata pia amani na ukimuona sasa na wakati ule unaweza kudhihirisha kwamba amebadilika.
“Kwa hiyo sitarajii kubadilika mimi kwa sababu ni kitu ambacho nimeamua na moyo wangu, sijashurutishwa na mtu na sina shinikizo lolote, kwa hiyo wategemee kumuona anapendeza zaidi kutoka ile hatua aliyokuwa nayo mpaka kumfikisha hapa na kwenda hatua nyingine ya kuwa kijana,”amesema Doreen.
Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema familia ya mke wake ilimtaka alipie mahari ya Sh4.2 milioni ambapo hadi sasa ameweza kulipa Sh1 milioni.
0 Comments