Na John Walter-Manyara.
Basi la abiria kampuni ya Mohamed Classic lenye namba T 643 DJP lililokuwa linatoka Arusha kwenda Kigoma limepata ajali ya kugongana na Fusso lenye namba T 380 DWF iliyokuwa inatokaTabora kwenda Moshi na kusababisha vifo vya watu wa 3 na majeruhi 26.
Ajali hiyo imetokea leo tarehe 24/5/2022 wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.
Akizungumza kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 2 kwenye basi na kifo cha mtu 1 kwenye fuso pamoja na kusababisha majeruhi 26 ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutokuheshimu alama za barabarani.
Hata hivyo jeshi hilo linamtafuta dereva wa basi hilo ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.
Majeruhi katika ajali hiyo, wanaume ni 14, wanawake 10 pamoja na watoto 2 ambao wamefikishwa katika Hospitali ya Tumaini, wilaya Hanang Mkoani Manyara.
Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa watumishi wa barabara kuzingatia sheria za usalama Barabarani ili kuepukana na ajali.
0 Comments