NA REBECA DUWE , TANGA.
Baadhi ya wafanya biashara wa kamba za la mkonge jijini Tanga wameimba serikali kuweza kuzuia uingizwaji wa kamba za plastiki nchini ili kuweza kukuza biashara ya kamba zinatokana zao la mkonge hapa nnchini .
Wakizungumza waandishi wa habari katika soko la ngamiani wafanyabishara hao walisema kuwa uingizwaji wa kamaba za palastiki kutoka nchini china umeweza kuwa kero kwa biashara zao za kamba za mkonge kwani kutoka bei zao wateja wengi wamekuwa wakikimbilia kununua bidhaa za plastiki.
Hassan Halfani ambye ni mfanyabiashara wa muda mrefu sokoni hapo alisema kuwa biashara zao zimeathiriwa na bidhaa hizo kwa kiasi kikubwa ni vyema serikali ikalifanyika kazi ombi lao ili na wao wafanye biashara.
Aliongeza kusema kwamba biashara ya zao la mkonge ni bishara inayojulikana Duniani kote kwa sasa hivyo kwa kuwa nchi ya Tanzania ni nchi ambayo inasifa ya kuwa kilimo cha mkonge ni vyema serikali ikaweka kipaumbele kwa zao hilo.
Hana Abasi na Karimu Ally ni wafanyara wa kamaba za mkonge katika soko la Ngamiani nao wameiomba serikali iwaangalie kwa jicho la tatu katika kuwaunga mkono kwa kuweza kutakaza kamba za plastiki kwani kamaba hizo inachangia katika uchafuzi wa mazingira.
Aidha walisema Kamba za mkonge ni kamba zinazotumika vizuri na ni rafiki wa mazingira kwani inapoisha huoza na kuwa rutuba katika ardhi hivyo kama serikali ione changamoto hii na kuweza kulitatua ili wao wawe kujikwamua kimaisha .
Awali akizungumza katibu mtenda wa chama cha mkonge Tanzania (THE SISAL ASSOCIATION OF TANZANI )(SAT)Raphael Ngalondwa alisema kuwa bidhaa za plastiki bado ni changamoto kubwa kwa wafanyabishara wa bidhaa za mkonge kutokana na bei za bidhaa hizo kuwa kubwa lakini bei za bidhaa pastiki kuwa rahisi.
Aidha alitoa rai kwa serikali kuangalia namna ambayo wanaweza kuwasaidia wananchi wake ambao wanafanya biashara kupitia bidhaa mkonge ambao ni sifa ya Tanzania na mkoa wa Tanga kwa ujumla.
0 Comments