F Taasisi Ya Mwera Foundation Yapongezwa. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Taasisi Ya Mwera Foundation Yapongezwa.


Na Timothy Itembe Mara.

Imeelezwa wanafunzi walisajiliwa katika madarasa ya MEMKWA wamepata mafanikio makubwa kutokana na mitihani yao ya Taifa ya msingi na kujiunga na Elimu ya Sekondari.


Pongezi hizo zilitajwa mbele ya mgeni rasimi,Afisa Tarafa Inano,Jaina Ibrahim Meena kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya juma la Elimu ya watu wazima halmashauri ya Tarime mjini na halmashauri ya Bunda yaliyiofanyika viwanja vya Chuo cha uwalimu Tarime(TTC).


Akisoma risala Afisa Elimu watu wazima na elimu nje ya mfumo rasimi halmashauri ya Bunda,Florence  Njiku alisema hadi sasa wanafunzi waliosajiliwa katika madarasa ya MEMKWA wamepata mafanikio makubwa kwani wengi wao wameweza kufaulu mitihani yao ya Taifa na kuhitimu elimu ya msingi vilevile kujiunga na elimu ya sekondari na hata elimu ya juu.


“Ndugu mgeni rasimi hali kadhalika elimu hii ya MEMKWA inaweza kuwasaidia watoto wa kike walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na matatizo mbalimbali kama vile kupata ujauzito katikati wakiendelea na masomo hali duni ya familia,maradhi,kuhama hama kwa familia,migogoro ya kifamilia,kwa sasa wasichana  wamekusanywa na kupewa mafunzo ya elimu ya sekondari na masomo ya ujasiliamali lengo ili waweze kuendesha maisha yao”alisema Njiku.


Kwa Tarime mji tuna idadi ya vituo vya MEMKWA 24 vyenye idadi ya wanafunzi 354 ikiwa 14 kati yao ni wanafunzi wenye mahitaji maalumu pia kwa halmashauri ya wilaya Bunda wanavituo vya MEMKWA vipatavyo 22 vyenye idadi ya wanafunzi 347 ikiwa 13 kati yao ni wanafunzi wenye mahitaji maalumu,Tarime mji tuna wanafunzi wa kike MESKWA 30 ambao mafunzo yao wanayapata katika shule ya sekondari Turwa vile vile kwa halmashauri ya Bunda wana wanafunzi wa kike 08 ambao mafunzo yao hupatia shule ya sekondari Chisorya alisema Njiku.


Afisa huyo alitumia nafasi hiyo kupongeza Taasisi ya Mwera Foundation kufanikisha maadhimisho hayo kwa michango mbalimbali ikiwemo kushiriki maadhimisho pamoja na kuchangia nguvu kazi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kupongeza serikali ya awamu ya sita ya Samia Suluhu Hassani kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi hususani katika swala la kutekeleza miradi kwa jamii ikiwemo ya elimu Bure.


Afisa huyo alimaliza kwa kusema kuwa elimu ya EWW inakabiliwa na uhaba wa madarasa kwa wanafunzi wa MEMKWA hivyo kupelekea wanafunzi hao kusomea katika madarasa ya wanafunzi wa elimu rasimi kwa kujumuishwa na wanafunzi wa kawaida hali inayowafanya wasiwe Uhuru katika kujifunza kutokana na numri waio kuwa mkubwa.Pia mwamko mdogo kwa jamii kunachangia kuhusiana na EWW ikiwemo MEMKWA,MESKWA na MUKEJA tunaomba serikali kuweza kuongeza madarasa na walimu [ia serikali kutenga Bajeti ya EWW ili kusaidia wahusika kufuatilia kwa lengo la kuweza kuelimisha jamii.


Kwa upande wake Meneja Tasisis ya Mwera Foundation,Mwalimu Mwita Samsoni Marwa alisema taasisi hiyo imekuja na mpango wa kuunga tamko la serikali katika kutoa elimu Bure kwa mwaka 2019/2024 kuwasaidia vijana kusoma Bure chuoni na zaidi ya vijana 300 wamenufaika.


Mwalimu huyo aliongeza kuwa tasisi yake inapokea wanafunzi waliomaliza kidato cha Nne wakiwemo watoto wa kike walioshindwa kubahatika  kuendelea na elimu ya juu na kuwapa kozi mbalimbali ili kupata mafunzo ya kuwawezesha kujiandaa kimaisha 


Mwalimu Julius Mboi kutoka Bunda ambaye anafundisha wanafunzi wa mahitaji maalumu wenye ulemavu wa usikivu alisema wanafunzi hao wanakabiliwa na upungufu wa vifaa mashuleni vya kufundishia.

Naye Mwalimu Getrude Kilaro kutoka shule ya msingi Turwa alisema kuna haja wazazi na walezi kutowaficha majumbani watoto wenye mahitaji maalumu badala yake wawalete shuleni kupata ili kupata elimu serikali imefungua milango kwa wanafunzi hao.


katika maadhimisho hayo Inapendekezwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu mitaala yao ya elimu itofautishwe na wanafunzi wa kawaida hususani wakati wa kutunga mitihani ya kumaliza darasa la saba na sekondari na kwingineko kutokana na upungufu walionao.


Naye Afisa Tarafa Inano,Martha Omahe  ambaye alimwakilisha mgeni rasimi alisema kuna haja watumishi kuendelea kuunga juhudi za serikali katika kufanya kazi walizoajiriwa na kuiletea maendeleo jamii inayowazunguka na serikali kwa ujumla.


Afisa huyo aliwataka wale wote walioshiriki maadhimisho hayo kwenda na kuwa kioo kwa jamii inayowazunguka na kuwa elimu walioipata isiishie kwenya viwanja vya maonyesho na kuwa Elimu waliyoipata waipeleke kwa jamii hususani katika swala zima la Elimu ya Ubunifu  wa miradi ya kujiajiri na kujitegemea  kuliko kuendelea kutegemea ajira serikalini wakati Ajira ni chache.

Post a Comment

0 Comments